John 20:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akamwambia, “Usinishike; sijaenda bado juu kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu uwaambie: Naenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamwambia, “Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akamwambia, “Hupaswi kunishika! Kwani bado sijapaa kwenda huko juu kwa Baba yangu. Lakini nenda ukawaambie wafuasi wangu maneno haya: ‘Ninarudi kwa Baba yangu ambaye pia ni Baba yenu. Ninarudi kwa Mungu wangu ambaye pia ni Mungu wenu.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akamwambia, “Usinishike; sijakwenda bado juu kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu uwaambie: nakwenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akamwambia, “Usinishike; sijaenda bado juu kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu uwaambie: naenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamwambia, “Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamwambia, “Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akamwambia, “Usinishike; sijaenda bado juu kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu uwaambie: Naenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akamwambia: Usiniguse! Kwani sijapaa bado kwenda kwake Baba. Lakini uende kwa ndugu zangu, uwaambie: Ninapaa kwenda kwa Baba yangu aliye hata Baba yenu na kwa Mungu wangu aliye hata Mungu wenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akamwambia: “Usinishike, kwa sababu sijapanda bado kwa Baba. Lakini kwenda kwa wandugu zangu na kuwaambia kwamba ninapanda kwa Baba yangu anayekuwa Baba yenu vilevile, anayekuwa Mungu wangu na Mungu wenu vilevile.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akamwambia, Usiniguse; kwa maana sijapaa kwa Baba yangu. Lakini enenda kwa ndugu zangu, ukawaambie, Ninapaa kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.