John 20:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ilikuwa jioni ya siku hiyo ya Jumapili. Wanafunzi walikuwa wamekutana pamoja ndani ya nyumba, na milango ilikuwa imefungwa kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi. Basi, Yesu akaja, akasimama kati yao, akawaambia, “Amani kwenu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilipokuwa jioni ya siku hiyo hiyo ya kwanza ya juma, wanafunzi wake walikuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa viongozi wa Wayahudi. Naye Isa akawatokea, akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ilikuwa siku ya Jumapili, na jioni ile wafuasi walikuwa pamoja. Nao walikuwa wamefunga milango kwa kuwa waliwaogopa viongozi wa Wayahudi. Ghafla, Yesu akawa amesimama pale katikati yao. Akasema, “Amani iwe nanyi!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ilikuwa jioni ya siku hiyo ya Jumapili. Wanafunzi walikuwa wamekutana pamoja ndani ya nyumba, na milango ilikuwa imefungwa kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi. Basi, Yesu akaja, akasimama kati yao, akawaambia, “Amani kwenu!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ilikuwa jioni ya siku hiyo ya Jumapili. Wanafunzi walikuwa wamekutana pamoja ndani ya nyumba, na milango ilikuwa imefungwa kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi. Basi, Yesu akaja, akasimama kati yao, akawaambia, “Amani kwenu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikawa jioni ya ile siku ya kwanza ya juma, wanafunzi wake walipokuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, Yesu aliwatokea, akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikawa jioni ya ile siku ya kwanza ya juma, wanafunzi wake walikuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi. Naye Isa aliwatokea, akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ilikuwa jioni ya siku hiyo ya Jumapili. Wanafunzi walikuwa wamekutana pamoja ndani ya nyumba, na milango ilikuwa imefungwa kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi. Basi, Yesu akaja, akasimama kati yao, akawaambia, “Amani kwenu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Siku ile ya kwanza ya juma kulipokuchwa, wanafunzi wakakutana, milango ya mle walimokuwa ikiwa imefungwa, maana waliwaogopa Wayuda. Mara Yesu akaja, akasimama katikati, akawaambia: Tengemaneni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Magaribi ya ile ile siku ya kwanza ya juma, wanafunzi walikusanyika katika nyumba na milango ilikuwa imefungwa, kwa sababu waliwaogopa wakubwa wa Wayuda. Mara moja Yesu akawatokea na kusimama katikati yao, akawaambia: “Amani kwenu!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ikawa jioni katika siku ile ya kwanza ya sabato, na milango imefungwa walipokuwapo wanafunzi kwa khofu ya Wayahudi, akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani kwenu.