John 20:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowasamehe, hawasamehewi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkimwondolea mtu yeyote dhambi zake, zitaondolewa; na yeyote msiyemwondolea dhambi zake, hazitaondolewa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mkisamehe dhambi zake mtu yeyote, dhambi zake hizo zitasamehewa. Kama kuna mtu yeyote ambaye hamtamsamehe dhambi zake, dhambi zake huyo hazitasamehewa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowaondolea, hawasamehewi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowasamehe, hawasamehewi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkimwondolea mtu ye yote dhambi zake, zitaondolewa na ye yote mtakayemfungia dhambi zake, zitafungiwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkimwondolea mtu yeyote dhambi zake, zitaondolewa, na yeyote msiyemwondolea dhambi zake, hazitaondolewa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowasamehe, hawasamehewi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu, mtakaowaondolea makosa, watakuwa wameondolewa. Nao watu, mtakaowafungia, watakuwa wamefungiwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote mutakaowasamehe zambi, watasamehewa; nao wote musiowasamehe, hawatasamehewa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia, wamefungiwa.