John 20:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Thoma, mmoja wa wale kumi na wawili (aitwaye Pacha), hakuwa pamoja nao wakati Yesu alipokuja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Tomaso (aliyeitwa Didimasi), mmoja wa wale kumi na wawili, hakuwa pamoja nao Isa alipokuja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini mmoja wa wale Thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tomaso (aliyeitwa Pacha) alikuwa ni mmoja wa wale kumi na mbili, lakini hakuwapo pamoja na wafuasi wengine Yesu alipokuja.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Thoma mmoja wa wale kumi na wawili (aitwaye Pacha), hakuwa pamoja nao wakati Yesu alipokuja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Thoma, mmoja wa wale kumi na wawili (aitwaye Pacha), hakuwa pamoja nao wakati Yesu alipokuja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Tomasi, aliyeitwa Didimasi, yaani, Pacha, mmoja wa wale kumi na wawili, hakuwa pamoja nao Yesu alipokuja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Tomaso, aliyeitwa Didimasi, yaani Pacha, mmoja wa wale kumi na wawili, hakuwa pamoja nao Isa alipokuja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mmoja wa wale Kumi na Wawili, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Thoma, mmoja wa wale kumi na wawili (aitwaye Pacha), hakuwa pamoja nao wakati Yesu alipokuja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Toma anayeitwa Pacha aliyekuwa mmoja wao wale kumi na wawili hakuwamo pamoja nao, Yesu alipokuja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini mmoja wa wale Thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Toma, anayeitwa “Pacha,” aliyekuwa mumoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, hakukuwa pamoja nao wakati Yesu alipokuja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tomaso, mmoja wa wathenashara aitwae Didumo, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu.