John 20:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Thoma akawaambia, “Nisipoona mikononi mwake alama za misumari na kutia kidole changu katika kovu hizo, na kutia mkono wangu ubavuni mwake, sitasadiki.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana Isa.” Lakini yeye akawaambia, “Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake, na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari, na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakamwambia, “Tulimwona Bwana.” Tomaso akasema, “Hiyo ni ngumu kuamini. Ninahitaji kuona makovu ya misumari katika mikono yake, niweke vidole vyangu ubavuni. Ndipo tu nitakapoamini.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Thoma akawaambia, “Nisipoona mikononi mwake alama za misumari, na kutia kidole changu katika kovu hizo, na kutia mkono wangu ubavuni mwake, sitasadiki.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Thoma akawaambia, “Nisipoona mikononi mwake alama za misumari na kutia kidole changu katika kovu hizo, na kutia mkono wangu ubavuni mwake, sitasadiki.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Lakini yeye akawaambia, “Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana Isa.” Lakini yeye akawaambia, “Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake, na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Thoma akawaambia, “Nisipoona mikononi mwake alama za misumari na kutia kidole changu katika kovu hizo, na kutia mkono wangu ubavuni mwake, sitasadiki.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wanafunzi wenzake walipomwambia: Tumemwona Bwana! akawajibu: Nisipoyaona makovu ya misumari maganjani mwake na kukitia kidole changu pale penye misumari, tena nisipoutia mkono wangu ubavuni mwake, sitamtegemea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafunzi wengine wakamwambia: “Tumemwona Bwana.” Lakini Toma akawajibu: “Nisipoona alama za misumari katika mikono yake na kutia kidole changu katika kovu za misumari ile, nami nisipoingiza vidole vyangu ndani ya ubavu wake, sitaamini.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Nisipoona mikononi mwake alama za misumari, na kutia kidole changu katika alama za misumari, na kutia mkono wangu uhavuni mwake, sitaamini kabisa.