John 20:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, baada ya siku nane hao wanafunzi walikuwa tena pamoja mle ndani, na Thoma alikuwa pamoja nao. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akaja, akasimama kati yao, akasema, “Amani kwenu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwa tena pamoja ndani ya nyumba, naye Tomaso alikuwa pamoja nao. Ndipo Isa akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Juma moja baadaye wafuasi walikuwemo katika nyumba ile tena, na Tomaso alikuwa pamoja nao. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akaja na kusimama katikati yao. Akasema, “Amani iwe nanyi!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, baada ya siku nane hao wanafunzi walikuwa tena pamoja mle ndani, na Thoma alikuwa pamoja nao. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akaja, akasimama kati yao, akasema, “Amani kwenu!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, baada ya siku nane hao wanafunzi walikuwa tena pamoja mle ndani, na Thoma alikuwa pamoja nao. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akaja, akasimama kati yao, akasema, “Amani kwenu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwa tena pamoja ndani ya nyumba, naye Tomasi alikuwa pamoja nao. Ndipo Yesu akaja milango ikiwa imefungwa na kusimama katikati yao akasema, “Amani iwe nanyi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwa tena pamoja ndani ya nyumba, naye Tomaso alikuwa pamoja nao. Ndipo Isa akaja milango ikiwa imefungwa na kusimama katikati yao akasema, “Amani iwe nanyi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, baada ya siku nane hao wanafunzi walikuwa tena pamoja mle ndani, na Thoma alikuwa pamoja nao. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akaja, akasimama kati yao, akasema, “Amani kwenu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwamo tena, naye Toma alikuwa yumo pamoja nao. Yesu akaja, milango ilipokuwa imefungwa, akasimama katikati, akasema: Tengemaneni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ilipotimia juma moja nyuma ya pale, wanafunzi wa Yesu wakakusanyika tena ndani ya nyumba ile ile, na mara hii Toma alikuwa pamoja nao. Ijapokuwa milango ilikuwa imefungwa, Yesu akawatokea tena, akasimama katikati yao na kusema: “Amani kwenu!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwamo ndani marra ya pili, na Tomaso pamoja nao. Yesu akaja, milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani kwenu.