John 20:31 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mpate kuwa na uhai kwa nguvu ya jina lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini hii imeandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Isa ndiye Al-Masihi, Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini haya yameandikwa ili muweze kuamini kwamba Yesu ni Masihi, Mwana wa Mungu. Kisha, kwa kuamini, mpate uzima kupitia jina lake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mpate kuwa na uzima kwa nguvu ya jina lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mpate kuwa na uhai kwa nguvu ya jina lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Isa ndiye Al-Masihi, Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini muwe na uzima kwa jina lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mpate kuwa na uhai kwa nguvu ya jina lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hivyo vimeandikwa, mpate kuyategemea, ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wake Mungu, tena mpate uzima katika Jina lake kwa kumtegemea.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini hii imeandikwa kusudi mupate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mupate uzima katika jina lake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
lakini hizi zimeandikwa mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.