John 20:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na kile kitambaa alichofungwa Yesu kichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwa pamoja na hiyo sanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Isa. Kitambaa hicho kilikuwa kimekunjwa peke yake, mbali na vile vitambaa vya kitani vya ile sanda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia aliiona nguo iliyokuwa imezungushwa kichwani kwa Yesu. Hii ilikuwa imekunjwa na kuwekwa upande mwingine tofauti na pale zilipokuwepo nguo za kitani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na kile kitambaa alichofungwa Yesu kichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwa pamoja na hiyo sanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na kile kitambaa alichofungwa Yesu kichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwa pamoja na hiyo sanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Yesu. Kitambaa hicho kilikuwa kimekunjwa mahali pa peke yake, mbali na vile vitambaa vya kitani vya ile sanda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Isa. Kitambaa hicho kilikuwa kimekunjwa mahali pa peke yake, mbali na vile vitambaa vya kitani vya ile sanda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwazongwa mbali mahali peke yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na kile kitambaa alichofungwa Yesu kichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwa pamoja na hiyo sanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini mharuma uliokuwa kichwani pake haukuwekwa pamoja na sanda, ila ulikuwa umekunjwa na kuwekwa mahali pake peke yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
vilevile akaona kitambaa kilichofunika kichwa cha Yesu. Kitambaa kile hakikuwekwa pamoja na vile vingine, lakini kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa peke yake pahali pengine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na ile leso iliyokuwa kichwani pake, haikuwekwa pamoja na vitambaa, bali imekunjwa, na kuwekwa mahali pa peke yake.