John 21:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Simoni Petro akapanda mashuani, akavuta hadi nchi kavu ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa 153. Na ingawa walikuwa wengi hivyo, wavu haukukatika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu ufuoni. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na watatu (153). Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Simoni Petro akapanda chomboni, akalivuta jarife pwani, limejaa samaki wakubwa, mia hamsini na watatu; na ijapokuwa ni wengi namna hiyo, jarife halikupasuka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Simoni Petro akaenda kwenye mashua na kuvuta wavu kuelekea ufukweni. Wavu huo ulikuwa umejaa samaki wakubwa, wapatao 153 kwa ujumla! Lakini pamoja na wingi wa samaki hao, nyavu hazikukatika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Simoni Petro akapanda mashuani, akavuta hadi nchi kavu ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa mia moja na hamsini na watatu. Na ingawa walikuwa wengi hivyo wavu haukukatika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Simoni Petro akapanda mashuani, akavuta hadi nchi kavu ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa 153. Na ingawa walikuwa wengi hivyo, wavu haukukatika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu pwani. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa 153. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu pwani. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa 153. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Simoni Petro akapanda katika mashua, akalivuta jarife pwani, limejaa samaki wakubwa, mia hamsini na watatu; na ijapokuwa ni wengi namna hiyo, jarife halikupasuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Simoni Petro akapanda mashuani, akavuta hadi nchi kavu ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa 153. Na ingawa walikuwa wengi hivyo, wavu haukukatika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Simoni Petero akapanda chomboni, akauvuta wavu ufukoni; wakawamo samaki wakubwa tu 153. Nao wavu haukupasuka, wangawa wengi kama hao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Simoni Petro akapanda chomboni, akalivuta jarife pwani, limejaa samaki wakubwa, mia hamsini na watatu; na ijapokuwa ni wengi namna hiyo, jarife halikupasuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Simoni Petro akapanda ndani ya chombo, akakokota wavu mpaka inchi kavu. Nao ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja makumi tano na tatu. Na ijapokuwa walikuwa wengi vile, wavu haukupasuka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Simon Petro akapanda chomboni, akalivuta jarife pwani, limejaa samaki kubwa, mia na khamsini na tatu: na ijapokuwa zilikuwa nyingi namna hii, jarife halikupasuka. Yesu akawaambia, Njoni mle.