John 21:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akawaambia, “Njoni mkafungue kinywa.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza: “Wewe ni nani?” maana walijua alikuwa Bwana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawaambia, “Njooni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wa wanafunzi aliyethubutu kumuuliza, “Wewe ni nani?” Walijua kuwa ni Bwana Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akawaambia, Njoni mfungue kinywa. Wala hakuna mtu katika wale wanafunzi aliyethubutu kumwuliza, U nani wewe? Wakijua ya kuwa ni Bwana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akawaambia, “Njooni mle.” Hakuna hata mfuasi mmoja aliyemwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua yeye alikuwa ni Bwana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akawaambia, “Njoni mkafungue kinywa.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza: “Wewe ni nani?” Maana walijua alikuwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akawaambia, “Njoni mkafungue kinywa.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza: “Wewe ni nani?” maana walijua alikuwa Bwana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawaambia, “Njoni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Kwa sababu walijua ya kuwa ni Bwana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawaambia, “Njooni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wa wanafunzi aliyethubutu kumuuliza, “Wewe ni nani?” Kwa sababu walijua ya kuwa ni Bwana Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akawaambia, Njooni mfungue kinywa. Wala hakuna mtu katika wale wanafunzi aliyethubutu kumwuliza, U nani wewe? Wakijua ya kuwa ni Bwana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akawaambia, “Njoni mkafungue kinywa.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza: “Wewe ni nani?” maana walijua alikuwa Bwana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yesu akawaambia: Njoni, mle! Miongoni mwao hao wanafunzi hakuwamo hata mmoja aliyejipa moyo wa kumwuliza: Wewe u nani? Walimjua, ya kuwa ndiye Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akawaambia, Njoni mfungue kinywa. Wala hakuna mtu katika wale wanafunzi aliyethubutu kumwuliza, U nani wewe? Wakijua ya kuwa ni Bwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawaambia: “Mukuje mukule.” Na hakuna hata mumoja kati ya wanafunzi aliyesubutu kumwuliza kwamba yeye ni nani, kwa maana walijua kwamba ni Bwana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala hapana mtu katika wale wanafunzi aliyethubutu kumwuliza, Wewe nani? wakijua ya kuwa ni Bwana.