John 21:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipokwisha kula, Yesu alimwuliza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohane! Je, wanipenda mimi kuliko hawa?” Naye akajibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza wanakondoo wangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokwisha kula, Isa akamuuliza Simoni Petro, “Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Isa akamwambia, “Lisha wana-kondoo wangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walipomaliza kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohana, je, unanipenda kuliko watu wote hawa wanavyonipenda?” Petro akajibu, “Ndiyo, Bwana, unajua kuwa nakupenda.” Kisha Yesu akamwambia, “Wachunge wanakondoo wangu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walipokwisha kula, Yesu alimwuliza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohane! Je, wanipenda mimi zaidi kuliko hawa?” Naye akajibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza wana kondoo wangu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipokwisha kula, Yesu alimwuliza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohane! Je, wanipenda mimi kuliko hawa?” Naye akajibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza wanakondoo wangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wana-kondoo wangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokwisha kula, Isa akamuuliza Simoni Petro, “Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Isa akamwambia, “Lisha wana-kondoo wangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipokwisha kula, Yesu alimwuliza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohane! Je, wanipenda mimi kuliko hawa?” Naye akajibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza wanakondoo wangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petero: Simoni wa Yohana, wanipenda kuliko hawa? Akamwambia: Ndio, Bwana, wewe unajua, ya kuwa ninakupenda. Akamwambia: Walishe wana kondoo wangu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro: “Simoni mwana wa Yoane, unanipenda mimi kuliko hawa?” Naye akamujibu: “Ndiyo, Bwana, unajua kama ninakupenda!” Yesu akamwambia: “Tunza wana-kondoo wangu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simon Petro, Simon wa Yohana, wanipenda kuliko bawa? Akamwambia, Naam, Bwana; wewe wajua ya kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana kondoo wangu.