John 21:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akamwambia mara ya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Petro akamjibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamuuliza tena, “Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?” Petro akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Isa akamwambia, “Chunga kondoo wangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa mara nyingine Yesu akamwambia, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akajibu, “Ndiyo, Bwana, wewe unajua kuwa nakupenda.” Kisha Yesu akasema, “Watunze kondoo wangu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha akamwambia mara ya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Petro akamjibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akamwambia mara ya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Petro akamjibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamwambia tena, “Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?” Petro akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Yesu akamwambia, “Chunga kondoo zangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamwambia tena, “Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?” Petro akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Isa akamwambia, “Chunga kondoo zangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akamwambia mara ya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Petro akamjibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipomwuliza tena mara ya pili: Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia: Ndio, Bwana, wewe unajua, ya kuwa ninakupenda. Akamwambia: Vichunge vikondoo vyangu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akamwuliza tena mara ya pili: “Simoni mwana wa Yoane, unanipenda?” Naye akamujibu: “Ndiyo, Bwana, unajua kama ninakupenda!” Yesu akamwambia tena: “Chunga kondoo wangu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamwambia marra ya pili, Simon wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Naam, Bwana; wewe wajua ya kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu.