John 21:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kweli nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kujifunga mshipi na kwenda kokote ulikotaka. Lakini utakapokuwa mzee utanyosha mikono yako, na mtu mwingine atakufunga na kukupeleka usikopenda kwenda.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amin, amin nakuambia, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka. Lakini utakapokuwa mzee, utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika na kukupeleka usipotaka kwenda.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ukweli ni huu, wakati ulipokuwa mdogo, ulijifunga mwenyewe mkanda wako kiunoni na kwenda ulikotaka. Lakini utakapozeeka, utainyoosha mikono yako, na mtu mwingine atakufunga mkanda wako. Watakuongoza kwenda mahali usikotaka kwenda.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kweli nakwambia, ulipokuwa kijana ulizoea kujifunga mshipi na kwenda kokote ulikotaka. Lakini utakapokuwa mzee utanyosha mikono yako, na mtu mwingine atakufunga na kukupeleka usikopenda kwenda.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kweli nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kujifunga mshipi na kwenda kokote ulikotaka. Lakini utakapokuwa mzee utanyosha mikono yako, na mtu mwingine atakufunga na kukupeleka usikopenda kwenda.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amin, amin nakuambia, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka, lakini utakapokuwa mzee utanyosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika na kukupeleka usipotaka kwenda.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amin, amin nakuambia, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka, lakini utakapokuwa mzee utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika na kukupeleka usipotaka kwenda.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kweli nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kujifunga mshipi na kwenda kokote ulikotaka. Lakini utakapokuwa mzee utanyosha mikono yako, na mtu mwingine atakufunga na kukupeleka usikopenda kwenda.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli kweli nakuambia: Ulipokuwa kijana ulijifunga mwenyewe, ukaenda, ulikotaka. Lakini utakapokuwa mzee utainyosha mikono yako, mwingine akuvike, akupeleke, usikotaka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninakuambia mambo ya kweli: wakati ulipokuwa kijana, ulijivalisha wewe mwenyewe na kwenda pahali ulipotaka. Lakini wakati utakapokuwa muzee, utanyoosha mikono yako na mutu mwingine atakuvalisha na kukupeleka pahali usipotaka.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Amin, amin, nakuambia, Ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga, ukienda ulikotaka; utakapokuwa mzee, utanyosha mikono yako, na mwingine atakufunga, atakuchukua usikotaka.