John 21:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Kwa kusema hivyo, alionesha jinsi Petro atakavyokufa na kumtukuza Mungu). Kisha akamwambia, “Nifuate.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alisema haya ili kuashiria aina ya kifo ambacho Petro angemtukuza nacho Mungu. Kisha Isa akamwambia Petro, “Nifuate!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
(Yesu alisema hivi kumwonyesha jinsi Petro atakavyokufa ili kumpa utukufu Mungu.) Kisha akamwambia Petro, “Nifuate!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
(Kwa kusema hivyo, alionyesha jinsi Petro atakavyokufa na kumtukuza Mungu.) Kisha akamwambia, “Nifuate.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
(Kwa kusema hivyo, alionesha jinsi Petro atakavyokufa na kumtukuza Mungu). Kisha akamwambia, “Nifuate.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu alisema haya ili kuashiria ni kifo cha aina gani Petro atakachomtukuza nacho Mungu. Kisha Yesu akamwambia Petro, “Nifuate!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alisema haya ili kuashiria ni kifo cha aina gani Petro atakachomtukuza nacho Mungu. Kisha Isa akamwambia Petro, “Nifuate!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema neno hilo kwa kuonesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
(Kwa kusema hivyo, alionesha jinsi Petro atakavyokufa na kumtukuza Mungu). Kisha akamwambia, “Nifuate.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Neno hili alilisema, amwonyeshe kufa, alikotakiwa, amtukuze Mungu nako. Alipokwisha kuyasema haya akamwambia; Nifuate!*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
(Yesu alisema maneno haya kwa kuonyesha kifo gani Petro atakachokufa na kumutukuza Mungu.) Kisha kusema maneno haya, Yesu akamwambia: “Unifuate!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasema hili kwa kuonyesha ni mauti gani atakayomtukuza Mungu. Na akiisha kusema haya, akamwambia, Nifuate.