John 21:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulipoanza kupambazuka, Yesu alisimama kando ya ziwa, lakini wanafunzi hawakujua kwamba alikuwa ni yeye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara baada ya kupambazuka, Isa akasimama ufuoni, lakini wanafunzi hawakumtambua kwamba alikuwa Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufuoni; walakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Asubuhi na mapema siku iliyofuata Yesu akasimama ufukweni mwa bahari. Hata hivyo wafuasi wake hawakujua kuwa alikuwa ni yeye Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulipoanza kupambazuka, Yesu alisimama kando ya ziwa, lakini wanafunzi hawakujua kwamba alikuwa yeye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulipoanza kupambazuka, Yesu alisimama kando ya ziwa, lakini wanafunzi hawakujua kwamba alikuwa ni yeye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara baada ya kupambazuka, Yesu akasimama ufuoni, lakini wanafunzi hawakumtambua kwamba alikuwa Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara baada ya kupambazuka, Isa akasimama ufuoni, lakini wanafunzi hawakumtambua kwamba alikuwa Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufuoni; lakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulipoanza kupambazuka, Yesu alisimama kando ya ziwa, lakini wanafunzi hawakujua kwamba alikuwa ni yeye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulipoanza kucha, Yesu alikuwa amesimama ufukoni, lakini wanafunzi hawakumjua, ya kuwa ndiye Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufuoni; walakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Asubui mapema, Yesu akaonekana kandokando ya ziwa, lakini wanafunzi hawakutambua kwamba ni yeye.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta assubuhi kulipokucha, Yesu akasimama ufukoni, walakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu.