John 3:34 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, maana Mungu humjalia mtu huyo Roho wake bila kipimo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humpa Roho wake pasipo kipimo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na kwamba Mungu alimtuma, na yeye huwaeleza watu yale yote Mungu aliyoyasema. Huyo Mungu humpa Roho kwa ujazo kamili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yule aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, maana Mungu humjalia mtu huyo Roho wake bila kipimo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, maana Mungu humjalia mtu huyo Roho wake bila kipimo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humtoa Roho pasipo kipimo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye aliyetumwa na Mwenyezi Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humtoa Roho pasipo kipimo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, maana Mungu humjalia mtu huyo Roho wake bila kipimo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwani aliyetumwa na Mungu huyasema maneno yake Mungu, naye Mungu haigawii Roho kwa kuipima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliyetumwa na Mungu anasema maneno ya Mungu, kwa sababu Mungu anamujaza Roho wake kwa uwingi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.