John 4:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo mama akasema, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji, nacho kisima ni kirefu; utapata wapi maji yenye uhai?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji ya uzima utayapata wapi?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwanamke akasema, “Bwana, utayapata wapi maji yaliyo hai? Kisima hiki kina chake ni kirefu sana, nawe huna kitu cha kuchotea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyo mama akasema, “Mheshimiwa, wewe huna chombo cha kutekea maji, nacho kisima ni kirefu; utapata wapi maji yaliyo hai?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo mama akasema, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji, nacho kisima ni kirefu; utapata wapi maji yenye uhai?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji ya uzima utayapata wapi?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji ya uzima utayapata wapi?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo mama akasema, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji, nacho kisima ni kirefu; utapata wapi maji yenye uhai?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamwambia: Bwana, hunacho cha kutekea, nacho kisima ni kirefu, basi, utayapata wapi hayo maji yenye uzima?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mwanamuke akamwambia: “Bwana, hauna chombo cha kutekea, na kisima ni kirefu sana. Basi umepata wapi maji ya uzima?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea na kisima kinakwenda chini sana; bassi, umeyapata wapi haya maji yaliyo hayi?