John 4:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Au, labda wewe wajifanya mkuu zaidi kuliko baba yetu Yakobo? Yeye alitupa sisi kisima hiki; na yeye mwenyewe, watoto wake na mifugo wake walikunywa maji ya kisima hiki.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Je, wewe ni mkuu kumzidi baba yetu Yakobo? Yeye ndiye aliyetupa kisima hiki. Yeye alikunywa kutoka kisima hiki, na wanawe, na wanyama wake wote.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Au, labda wewe wajifanya mkuu kuliko babu yetu Yakobo? Yeye alitupa sisi kisima hiki; na yeye mwenyewe, watoto wake na mifugo yake walikunywa maji ya kisima hiki.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Au, labda wewe wajifanya mkuu zaidi kuliko baba yetu Yakobo? Yeye alitupa sisi kisima hiki; na yeye mwenyewe, watoto wake na mifugo wake walikunywa maji ya kisima hiki.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Au, labda wewe wajifanya mkuu zaidi kuliko baba yetu Yakobo? Yeye alitupa sisi kisima hiki; na yeye mwenyewe, watoto wake na mifugo wake walikunywa maji ya kisima hiki.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Wewe u mkubwa kuliko baba yetu Yakobo aliyetupa kisima hiki? Naye alikunywa humu mwenyewe na watoto wake na nyama wake wa kufuga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Babu yetu Yakobo ndiye aliyetupa sisi kisima hiki, hata yeye mwenyewe pamoja na wana wake na nyama wake walikunywa maji yake. Wewe unajiona kuwa mukubwa kuliko Yakobo?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Je! wewe u mkubwa kuliko baba yetu Yakobo aliyetupa kisima hiki, nae mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na nyama zake?