John 4:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Babu zetu waliabudu juu ya mlima huu, lakini nyinyi mwasema kwamba mahali pa kumwabudia Mungu ni kule Yerusalemu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baba zetu waliabudu katika mlima huu. Lakini ninyi Wayahudi mnasema kuwa Yerusalemu ndipo mahali ambapo watu wanapaswa kuabudia.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Babu zetu waliabudu juu ya mlima huu, lakini ninyi mwasema kwamba mahali pa kumwabudu Mungu ni kule Yerusalemu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Babu zetu waliabudu juu ya mlima huu, lakini nyinyi mwasema kwamba mahali pa kumwabudia Mungu ni kule Yerusalemu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Babu zetu waliabudu juu ya mlima huu, lakini nyinyi mwasema kwamba mahali pa kumwabudia Mungu ni kule Yerusalemu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baba zetu walitambikia mlimani huku, nanyi husema: Yerusalemu ndipo, panapopasa kupatambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Babu zetu walimwabudu Mungu juu ya mulima huu, lakini ninyi Wayuda munasema kama Yerusalema ni pahali pa kumwabudia Mungu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baba zetu waliabudu katika mlima huu, na ninyi husema kwamba Yerusalemi ni mahali patupasapo kuabudia.