John 4:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wakati waja, tena umekwisha wasili, ambapo wenye kuabudu wa kweli watamwabudu Baba katika roho na ukweli. Maana Baba anawataka watu wanaomwabudu namna hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba anawatafuta watu wanaomwabudu kwa namna hii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini wakati unakuja wenye nia halisi ya kuabudu watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa hakika, wakati huo sasa umekwishafika. Na hao ndiyo watu ambao Baba anataka wamwabudu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wanaoabudu kweli, watamwabudu Baba kwa nguvu ya Roho; watu wanaomwabudu hivyo ndio Baba anaotaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wakati waja, tena umekwisha wasili, ambapo wenye kuabudu wa kweli watamwabudu Baba katika roho na ukweli. Maana Baba anawataka watu wanaomwabudu namna hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wakati waja, tena umekwisha wasili, ambapo wenye kuabudu wa kweli watamwabudu Baba katika roho na ukweli. Maana Baba anawataka watu wanaomwabudu namna hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini saa inakuja, tena sasa iko, wenye kutambika kweli watakapomtambikia Baba kiroho na kikweli, kwani naye Baba huwataka wanaomtambikia hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kutakuwa wakati, nao umekwisha kutimia, wale wanaoabudu kwa kweli watakapomwabudu Baba katika roho na ukweli; kwa maana Baba anataka watu wanaoabudu kwa namna ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini saa inakuja, na sasa ipo, ambayo wenye ibada khalisi watamwabudu Baba katika roho na kweli: kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.