John 4:27 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo wanafunzi wake wakarudi, wakastaajabu sana kuona anaongea na mwanamke. Lakini hakuna mtu aliyesema: “Unataka nini?” au, “Kwa nini unaongea na mwanamke?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au, “Kwa nini unazungumza naye?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara hiyo wakaja wanafunzi wake, wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hakuna aliyesema, Unatafuta nini? Au, Mbona unasema naye?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati huo huo wafuasi wa Yesu wakarudi toka mjini. Nao walishangaa kwa sababu walimwona Yesu akiongea na mwanamke. Lakini hakuna aliyemwuliza yule mwanamke, “Unataka nini?” Wala Yesu, “Kwa nini unaongea naye?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo wanafunzi wake wakarudi, wakastaajabu sana kuona anaongea na mwanamke. Lakini hakuna mtu aliyesema: “Unataka nini?” au, “Kwa nini unaongea na mwanamke?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo wanafunzi wake wakarudi, wakastaajabu sana kuona anaongea na mwanamke. Lakini hakuna mtu aliyesema: “Unataka nini?” au, “Kwa nini unaongea na mwanamke?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemwuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara hiyo wakaja wanafunzi wake, wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hakuna aliyesema, Unatafuta nini? Au, Mbona unasema naye?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo wanafunzi wake wakarudi, wakastaajabu sana kuona anaongea na mwanamke. Lakini hakuna mtu aliyesema: “Unataka nini?” au, “Kwa nini unaongea na mwanamke?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo wanafunzi wake wakaja, wakashangaa, ya kuwa anasema na mwanamke; lakini hakuna aliyeuliza: Watafuta nini? au: Wasemaje naye?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara hiyo wakaja wanafunzi wake, wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hakuna aliyesema, Unatafuta nini? Au, Mbona unasema naye?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Saa ile ile wanafunzi wa Yesu wakarudi, nao wakashangaa kumwona akisemezana na mwanamuke. Lakini hakuna mumoja wao aliyemwuliza yule mwanamuke kwamba anataka nini au kumwuliza Yesu kwamba sababu gani anasema naye.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra hiyo wakaja wanafunzi wake wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hapana aliyesema, Unatafuta nini? au, Kwa nini unasema nae?