John 4:35 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi mwasema: ‘Bado miezi minne tu, na wakati wa mavuno utafika!’ Lakini mimi nawaambieni, angalieni mkaone jinsi mashamba yalivyo tayari kuvunwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune’? Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnapopanda mimea, huwa mnasema, ‘Bado miezi minne ya kusubiri kabla ya kuvuna mazao.’ Lakini mimi ninawaambia, yafumbueni macho yenu na kuyaangalia mashamba. Sasa yako tayari kuvunwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi mwasema: Bado miezi minne tu, na wakati wa mavuno utafika! Lakini mimi nawaambieni, yatazameni mashamba; mazao yako tayari kuvunwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi mwasema: ‘Bado miezi minne tu, na wakati wa mavuno utafika!’ Lakini mimi nawaambieni, angalieni mkaone jinsi mashamba yalivyo tayari kuvunwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune?’ Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune?’ Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yanakuja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi mwasema: ‘Bado miezi minne tu, na wakati wa mavuno utafika!’ Lakini mimi nawaambieni, angalieni mkaone jinsi mashamba yalivyo tayari kuvunwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi hamsemi: Iko miezi minne bado, mavuno yatakapokuwapo? Tazameni, nawaambiani: Yainueni macho yenu, myatazame mashamba! Yamekwisha kuwa meupe, yavunwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Si ninyi munazoea kusema: ‘Kunabaki miezi mine kuwe mavuno’? Lakini mimi ninawaambia, muinue macho, muangalie mashamba; mimea imekomaa, nayo ni tayari kwa kuvunwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hamsemi ninyi, Imebaki miezi mine bado, ndipo yaja mavuno? Nami nawaambieni, Inueni macho yenu, mkayatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe tayari kwa mavuno.