John 4:38 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi nimewatuma mkavune mavuno ambayo hamkuyatolea jasho; wengine walifanya kazi, lakini nyinyi mnafaidika kutokana na jasho lao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda. Wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mimi niliwatuma kukusanya mazao ambayo ninyi hamkuyahangaikia. Wengine waliyahangaikia, nanyi mnapata faida kutokana na juhudi na kazi yao.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mimi nimewatuma mkavune mavuno ambayo hamkuyatolea jasho, wengine walifanya kazi, lakini ninyi mnafaidika kutokana na jasho lao.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi nimewatuma mkavune mavuno ambayo hamkuyatolea jasho; wengine walifanya kazi, lakini nyinyi mnafaidika kutokana na jasho lao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi niliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi nimewatuma mkavune mavuno ambayo hamkuyatolea jasho; wengine walifanya kazi, lakini nyinyi mnafaidika kutokana na jasho lao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi naliwatuma, mvune, msiyoyafanyia kazi; wengine wamefanya kazi, ninyi mkaingia kazini mwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi niliwatuma ninyi katika shamba kuvuna mavuno ambayo hamukusumbukia; wengine waliyasumbukia, nanyi mumepata faida ya kazi yao.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mimi naliwatuma myavune msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.