John 4:39 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wasamaria wengi wa kijiji kile walimwamini kwa sababu ya maneno aliyosema huyo mama: “Ameniambia mambo yote niliyofanya.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wasamaria wengi katika mji ule wakamwamini Isa kwa sababu ya ushuhuda wa yule mwanamke alipowaambia kwamba, “Ameniambia kila kitu nilichotenda.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wasamaria wengi katika mji huo wakamwamini Yesu. Wakaamini kutokana na yale ambayo walisikia yule mwanamke akiwaambia juu ya Yesu. Aliwaambia, “Yeye amenieleza mambo yote niliyowahi kuyafanya.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wasamaria wengi wa kijiji kile waliamini kwa sababu ya maneno aliyosema huyo mama: “Ameniambia mambo yote niliyofanya.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wasamaria wengi wa kijiji kile walimwamini kwa sababu ya maneno aliyosema huyo mama: “Ameniambia mambo yote niliyofanya.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wasamaria wengi kutoka katika mji ule wakamwamini Yesu kwa sababu ya ushuhuda wa yule mwanamke alipowaambia kwamba, “Ameniambia kila jambo nililotenda.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wasamaria wengi katika mji ule wakamwamini Isa kwa sababu ya ushuhuda wa yule mwanamke alipowaambia kwamba, “Ameniambia kila kitu nilichotenda.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wasamaria wengi wa kijiji kile walimwamini kwa sababu ya maneno aliyosema huyo mama: “Ameniambia mambo yote niliyofanya.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Wasamaria wengi wa mji ule wakamtegemea kwa ajili ya neno, yule mwanamke alilomshuhudia kwamba: Ameniambia yote, niliyoyafanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wasamaria wengi wa muji ule walimwamini Yesu kwa sababu ya maneno ya yule mwanamuke aliposhuhudia hivi: “Aliniambia mambo yote niliyotenda.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na katika mji ule Wasamaria wengi wakaamini kwa sababu ya maneno ya yule mwananike, aliposhuhudu, kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda.