John 4:45 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, alipofika Galilaya, Wagalilaya wengi walimkaribisha. Maana nao pia walikuwa kwenye sikukuu ya Pasaka, wakayaona mambo yote Yesu aliyotenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipofika Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha, kwani walikuwa wameona yale aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Pasaka. Kwa maana wao pia walikuwa wamehudhuria hiyo Sikukuu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi alipotoka Galilaya, Wagalilaya walimpokea; kwa kuwa wameyaona mambo yote aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu; maana hao nao waliiendea sikukuu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alipofika Galilaya, watu wa pale walimkaribisha. Hao walikuwepo kwenye sikukuu ya Pasaka kule Yerusalemu na waliona kila kitu alichofanya huko.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, alipofika Galilaya, Wagalilaya wengi walimkaribisha. Maana nao pia walikuwa kwenye sikukuu ya Pasaka, wakayaona mambo yote Yesu aliyotenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, alipofika Galilaya, Wagalilaya wengi walimkaribisha. Maana nao pia walikuwa kwenye sikukuu ya Pasaka, wakayaona mambo yote Yesu aliyotenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipofika Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha, kwani walikuwa wameona yale aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Pasaka. Kwa maana wao pia walikuwa wamehudhuria kwenye hiyo Sikukuu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipofika Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha, kwani walikuwa wameona yale aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Pasaka. Kwa maana wao pia walikuwa wamehudhuria hiyo Sikukuu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi alipotoka Galilaya, Wagalilaya walimpokea; kwa kuwa wameyaona mambo yote aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu; maana hao nao waliiendea sikukuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, alipofika Galilaya, Wagalilaya wengi walimkaribisha. Maana nao pia walikuwa kwenye sikukuu ya Pasaka, wakayaona mambo yote Yesu aliyotenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipofika Galilea, Wagalilea wakampokea, kwani walikuwa wameyaona yote, aliyoyatenda Yerusalemu siku za sikukuu; kwani nao walikuwa wamekwenda kule siku za sikukuu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi alipotoka Galilaya, Wagalilaya walimpokea; kwa kuwa wameyaona mambo yote aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu; maana hao nao waliiendea sikukuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
lakini alipofika Galilaya, wakaaji wa kule wakamupokea, kwa maana wao vilevile walikuwa Yerusalema kwa sikukuu ya Pasaka, nao waliona mambo yote aliyofanya kule.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi alipofika Galilaya Wagalilaya wakampokea, kwa kuwa wameona mambo yote aliyoyatenda Yerusalemi wakati wa siku kuu; maana hao nao waliendea siku kuu.