John 4:46 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alifika tena huko mjini Kana, mkoani Galilaya, mahali alipogeuza maji kuwa divai. Kulikuwa na ofisa mmoja aliyekuwa na mtoto mgonjwa huko Kafarnaumu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Isa akafika tena Kana ya Galilaya, kule alikuwa amebadili maji kuwa divai. Kulikuwa na afisa mmoja wa mfalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye Yesu akaenda tena kutembelea Kana huko Galilaya. Kana ni mahali alikoyabadili maji kuwa divai. Mmoja wa maafisa muhimu wa mfalme alikuwa anaishi katika mji wa Kapernaumu. Mwanawe afisa huyu alikuwa mgonjwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alifika tena huko mjini Kana, mkoani Galilaya, mahali alipogeuza maji kuwa divai. Kulikuwa na ofisa mmoja aliyekuwa na mtoto mgonjwa huko Kafarnaumu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alifika tena huko mjini Kana, mkoani Galilaya, mahali alipogeuza maji kuwa divai. Kulikuwa na ofisa mmoja aliyekuwa na mtoto mgonjwa huko Kafarnaumu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Yesu akaja tena mpaka Kana ya Galilaya, kule alikokuwa amebadili maji kuwa divai. Huko kulikuwako na mtu mmoja afisa wa kifalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Isa akaja tena mpaka Kana ya Galilaya, kule alikokuwa amebadili maji kuwa divai. Huko kulikuwepo na afisa mmoja wa mfalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na ofisa mmoja ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alifika tena huko mjini Kana, mkoani Galilaya, mahali alipogeuza maji kuwa divai. Kulikuwa na ofisa mmoja aliyekuwa na mtoto mgonjwa huko Kafarnaumu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akafika tena Kana wa Galilea, alikogeuza maji kuwa mvinyo. *Kulikuwa na mtu wa kifalme aliyeuguliwa na mwana wake huko Kapernaumu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Yesu akarudi tena Galilaya katika muji Kana, pahali alipogeuza maji kuwa divai. Kule kulikuwa mukubwa mumoja wa serikali, aliyekuwa na mwana mugonjwa katika muji Kapernaumu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi akafika tena Kana ya Galilaya, hapo alipofanya maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja, ana mwana hawezi Kapernaum.