John 4:47 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, huyo ofisa aliposikia kuwa Yesu alikuwa ametoka Yudea na kufika Galilaya, alimwendea akamwomba aende kumponya mtoto wake aliyekuwa mgonjwa mahututi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyo mtu aliposikia kwamba Isa alikuwa amewasili Galilaya kutoka Yudea, alimwendea na kumsihi aende akamponye mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa kufani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Afisa huyo akasikia kwamba Yesu alikuwa amekuja kutoka Uyahudi na sasa yuko Galilaya. Hivyo akamwendea Yesu na kumsihi aende Kapernaumu kumponya mwanawe, aliyekuwa mahututi sana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, huyo ofisa aliposikia kuwa Yesu alikuwa ametoka Yudea na kufika Galilaya, alimwendea akamwomba aende kumponya mtoto wake aliyekuwa mgonjwa mahututi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, huyo ofisa aliposikia kuwa Yesu alikuwa ametoka Yudea na kufika Galilaya, alimwendea akamwomba aende kumponya mtoto wake aliyekuwa mgonjwa mahututi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyo mtu aliposikia kwamba Yesu alikuwa amewasili Galilaya kutoka Uyahudi, alimwendea na kumwomba ili aje kumponya mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyo mtu aliposikia kwamba Isa alikuwa amewasili Galilaya kutoka Uyahudi, alimwendea na kumwomba ili aje kumponya mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Yudea mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa karibu kufa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, huyo ofisa aliposikia kuwa Yesu alikuwa ametoka Yudea na kufika Galilaya, alimwendea akamwomba aende kumponya mtoto wake aliyekuwa mgonjwa mahututi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyo aliposikia, ya kuwa Yesu ametoka Yudea, akafika Galilea, akaondoka, akamwendea, akambembeleza, ashuke, amponye mwanawe, kwani alitaka kufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa kufani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati aliposikia kwamba Yesu amefika Galilaya toka Yudea, mukubwa huyu akamwendea, akamusihi aende Kapernaumu kumuponyesha mwana wake, aliyekuwa karibu kufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Huyu aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Yahudi hatta Galilaya, akamwendea, akamsihi ashuke akamponye mwana wake; kwa maana alikuwa kufani.