John 4:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu na shamba ambalo Yakobo alikuwa amempa mwanawe, Yosefu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yusufu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akiwa Samaria Yesu akafika katika mji wa Sikari, ulio karibu na shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yusufu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu na shamba ambalo Yakobo alikuwa amempa mwanawe, Yosefu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu na shamba ambalo Yakobo alikuwa amempa mwanawe, Yosefu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yosefu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yusufu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akafika katika mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu na shamba ambalo Yakobo alikuwa amempa mwanawe, Yosefu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Akafika penye mji wa Samaria, jina lake Sikari, ulio karibu ya kiunga, Yakobo alichompa mwanawe Yosefu;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akafika karibu na muji mumoja wa Samaria unaoitwa Sikari, uliokuwa karibu na shamba lile Yakobo alilomupa mwana wake Yosefu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi akafika mji wa Samaria, uitwao Sukar, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusuf mwanawe.