John 4:50 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akamwambia, “Nenda tu, mwanao ataishi.” Huyo mtu akaamini maneno ya Yesu, akaenda zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamjibu, “Nenda zako, mwanao yu hai.” Yule afisa akaamini yale maneno Isa aliyomwambia, akaenda zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akajibu, “Nenda, mwanao ataishi.” Mtu huyo akayaamini maneno Yesu aliyomwambia na akaenda nyumbani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akamwambia, “Nenda tu, mwanao yu mzima.” Huyo mtu akaamini maneno ya Yesu, akaenda zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akamwambia, “Nenda tu, mwanao ataishi.” Huyo mtu akaamini maneno ya Yesu, akaenda zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamjibu, “Enenda zako, mwanao yu hai.” Yule afisa akaamini yale maneno Yesu aliyomwambia, akaondoka akaenda zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamjibu, “Enenda zako, mwanao yu hai.” Yule afisa akaamini yale maneno Isa aliyomwambia, akaondoka akaenda zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akamwambia, Nenda; mwanao yu hai. Mtu yule akaliamini lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akamwambia, “Nenda tu, mwanao ataishi.” Huyo mtu akaamini maneno ya Yesu, akaenda zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akamwambia: Jiendee, mwana wako yuko mzima! Yule mtu akalitegemea neno, Yesu alilomwambia, akaenda zake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akamwambia: “Kwenda tu, mwana wako ni muzima.” Mutu yule akaamini neno Yesu alilosema, naye akaondoka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akamwambia, Shika njia yako: mwana wako yu hayi. Mtu yule akaliamini lile neno aliloambiwa na Yesu, akashika njia.