John 4:52 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akawauliza saa mtoto alipopata nafuu; nao wakamwambia, “Jana saa saba mchana, homa ilimwacha.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana saa saba, ndipo homa iliisha.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa hajambo; nao wakamwambia, Jana, saa saba, homa ilimwacha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu huyo akauliza, “Ni wakati gani mwanangu alipoanza kupata nafuu?” Wakajibu, “Ilikuwa jana saa saba mchana homa ilipomwacha.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye akawauliza saa mtoto alipopata nafuu; nao wakamwambia, “Jana saa saba mchana, homa ilimwacha.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akawauliza saa mtoto alipopata nafuu; nao wakamwambia, “Jana saa saba mchana, homa ilimwacha.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa na nafuu; nao wakamwambia, Jana, saa saba, homa ilimwacha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akawauliza saa mtoto alipopata nafuu; nao wakamwambia, “Jana saa saba mchana, homa ilimwacha.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawauliza saa, alipoanzia kuwa hajambo kidogo. Walipomwambia: Jana saa saba joto limemtoka,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa hajambo; nao wakamwambia, Jana, saa saba, homa ilimwacha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu akawauliza saa gani mutoto alipoanza kujisikia vizuri. Nao wakamujibu: “Yeye alipona homa jana muchana saa saba.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi akawauliza khabari ya saa alipoanza kuwa hajambo. Bassi wakamwamhia, Jana, saa saba, homa ilimwacha.

Recommended Reading