John 4:53 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo baba akakumbuka kwamba ilikuwa ni saa ileile ambapo Yesu alimwambia: “Mwanao ataishi.” Hapo yeye akaamini pamoja na jamaa yake yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo baba wa huyo mtoto akakumbuka kuwa huo ndio wakati Isa alikuwa amemwambia, “Mwanao yu hai.” Kwa hiyo yeye na wote wa nyumbani mwake wakamwamini Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baba yake akatambua kuwa saa saba kamili ulikuwa ndiyo ule wakati aliposema, “Mwanao ataishi.” Hivyo afisa huyo na kila mmoja katika nyumba yake wakamwamini Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyo baba akakumbuka kwamba ilikuwa ni saa ileile ambapo Yesu alimwambia: “Mwanao yu mzima.” Basi, yeye akaamini pamoja na jamaa yake yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo baba akakumbuka kwamba ilikuwa ni saa ileile ambapo Yesu alimwambia: “Mwanao ataishi.” Hapo yeye akaamini pamoja na jamaa yake yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo baba wa huyo mtoto akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Yesu alikuwa amemwambia, “Mwanao yu hai.” Kwa hiyo yeye, pamoja na wote wa nyumbani mwake wakamwamini Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo baba wa huyo mtoto akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Isa alikuwa amemwambia, “Mwanao yu hai.” Kwa hiyo yeye, pamoja na wote wa nyumbani mwake wakamwamini Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo baba akakumbuka kwamba ilikuwa ni saa ileile ambapo Yesu alimwambia: “Mwanao ataishi.” Hapo yeye akaamini pamoja na jamaa yake yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
baba akatambua, ya kuwa ni saa ileile, Yesu alipomwambia: Mwana wako yuko mzima. Ndipo, yeye nao waliokuwamo mwake walipomtegemea wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi baba yule akatambua kama ilikuwa ni saa ile ile Yesu alipomwambia kwamba mwana wake ni muzima. Basi yeye na jamaa yake yote wakamwamini Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi baba yake akafahamu ya kuwa ni saa ileile aliyoambiwa na Yesu, Mwana wako yu hayi. Akaamini yeye na nyumba yake yote.