John 4:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisima cha Yakobo kilikuwa huko. Naye Isa alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mahali hapo ndipo kilikuwapo kisima cha Yakobo. Kutokana na safari yake kuwa ndefu Yesu alichoka, hivyo akakaa chini kando ya kisima. Nayo ilikuwa saa sita adhuhuri.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huko ndiko kulikokuwa na kile kisima cha Yakobo. Naye Yesu alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huko ndiko kulikokuwa na kile kisima cha Yakobo. Naye Isa alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Kwa hivyo, Yesu alivyokuwa amechoka kwa mwendo, akakaa pale kisimani; ilikuwa kama saa sita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pale kulikuwa kisima kilichokuwa cha Yakobo. Yesu akaikaa kwa ukingo wa kisima, kwa sababu alikuwa amechoka na safari. Ilikuwa karibu na saa sita za muchana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Bassi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Ilikuwa yapata saa sita.