John 5:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, Mwana hawezi kufanya jambo lolote peke yake. Yeye aweza tu kufanya lile analomwona Baba yake akifanya, kwa maana lolote afanyalo Baba, Mwana pia hufanya vivyo hivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Yesu akajibu, “Hakika nawaambieni kuwa Mwana hawezi kufanya chochote peke yake. Bali hufanya tu yale anayoona Baba yake anayafanya. Kwa maana Mwana hufanya mambo ambayo Baba huyafanya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawaambia, “Amin, amin, nawaambia, Mwana hawezi kufanya jambo lo lote peke yake, yeye aweza tu kufanya lile analomwona Baba yake akifanya, kwa maana lo lote afanyalo Baba, Mwana pia hufanya vivyo hivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, Mwana hawezi kufanya jambo lolote peke yake, yeye aweza tu kufanya lile analomwona Baba yake akifanya, kwa maana lolote afanyalo Baba, Mwana pia hufanya vivyo hivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo anamwona Baba akilitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Yesu akajibu, akawaambia: Kweli kweli nawaambiani: Hakuna, Mwana awezacho kukifanya kwa nguvu yake, asipokuwa amemwona Baba, anavyokifanya. Kwani yule anavyovifanya, hivyo naye Mwana huvifanya vile vile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Yesu akaongeza kuwaambia Wayuda: “Kweli, kweli, ninawaambia: Mwana hawezi kufanya kitu kwa mafikiri yake mwenyewe; anafanya tu kile ambacho anaona Baba akifanya. Na mambo yote Baba anayofanya, Mwana anayafanya vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Mwana hawezi kutenda neno kwa nafsi yake, illa lile amwonalo Baba analitenda; kwa maana yote atendayo yeye, hayo na Mwana ayatenda vilevile.