John 5:42 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini nawajua nyinyi, najua kwamba upendo kwa Mungu haumo mioyoni mwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
lakini mimi ninawafahamu. Ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hata hivyo ninawajua ninyi, na ninajua kwamba hamna upendo kwa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini nawajua ninyi, najua kwamba upendo kwa Mungu haumo mioyoni mwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini nawajua nyinyi, najua kwamba upendo kwa Mungu haumo mioyoni mwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini nawajua nyinyi, najua kwamba upendo kwa Mungu haumo mioyoni mwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini nimewatambua ninyi, ya kuwa hamnao upendo wa Mungu mioyoni mwenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninawajua ninyi kwamba hamumupendi Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.