John 5:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye alipomwona huyo mtu amelala hapo na kujua kwamba alikuwa amekaa hapo kwa muda mrefu, akamwuliza, “Je, wataka kupona?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alipomwona akiwa amelala hapo, na akijua amekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu, akamwambia, “Je, wataka kuponywa?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alimwona akiwa amelala hapo na kutambua kuwa amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu sana. Hivyo akamwuliza, “Je, unataka kuwa mzima?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye alipomwona huyo mtu amelala hapo, akatambua kwamba alikuwa amekaa hapo kwa muda mrefu, akamwuliza, “Je, wataka kupona?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye alipomwona huyo mtu amelala hapo na kujua kwamba alikuwa amekaa hapo kwa muda mrefu, akamwuliza, “Je, wataka kupona?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu alipomwona akiwa amelala hapo, naye akijua kuwa amekuwako hapo kwa muda mrefu, akamwambia, “Je, wataka kuponywa?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alipomwona akiwa amelala hapo, naye akijua kuwa amekuwa hapo kwa muda mrefu, akamwambia, “Je, wataka kuponywa?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa katika hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye alipomwona huyo mtu amelala hapo na kujua kwamba alikuwa amekaa hapo kwa muda mrefu, akamwuliza, “Je, wataka kupona?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu alipomwona huyo, anavyolala, akatambua, ya kuwa imemwishia hapo miaka mingi, akamwambia: Unataka kuwa mzima?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Yesu alipomwona akilala na kutambua kwamba amekuwa mugonjwa kwa muda wa siku nyingi, akamwuliza: “Unataka kupona?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu alipomwona huyu amelala, akijua ya kuwa amekuwa hali hii siku nyingi, akamwambia, Wataka kuwa nizima?