John 6:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akasema, “Waketisheni watu.” Palikuwa na nyasi tele mahali hapo. Basi, watu wakaketi, jumla yapata wanaume 5,000.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akasema, “Waketisheni watu chini.” Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi (palikuwa na wanaume wapatao elfu tano).
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akasema, Waketisheni watu. Na mahali pale palikuwa na majani tele. Basi watu waume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akasema, “Mwambieni kila mtu akae chini.” Sehemu hiyo ilikuwa yenye nyasi nyingi, na wanaume wapatao 5,000 walikaa hapo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akasema, “Waketisheni watu.” Palikuwa na nyasi tele mahali hapo. Basi, watu wakaketi, jumla yapata wanaume elfu tano.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akasema, “Waketisheni watu.” Palikuwa na nyasi tele mahali hapo. Basi, watu wakaketi, jumla yapata wanaume 5,000.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akasema, “waketisheni watu chini.” Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi, palikuwa na wanaume 5,000.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akasema, “Waketisheni watu chini.” Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi. Palikuwa na wanaume wapatao 5,000.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akasema, Waketisheni watu. Na mahali pale palikuwa na majani tele. Basi wanaume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akasema, “Waketisheni watu.” Palikuwa na nyasi tele mahali hapo. Basi, watu wakaketi, jumla yapata wanaume 5,000.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akasema: Wakalisheni watu! maana mahali pale palikuwa na majani mengi; waliokaa waume tu walikuwa kama 5000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akasema, Waketisheni watu. Na mahali pale palikuwa na majani tele. Basi watu waume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akasema: “Muwaambie watu waikae chini.” (Pale kulikuwa majani mengi.) Basi wakaikaa chini; na hesabu ya wanaume tu ilikuwa yapata elfu tano.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akasema, Waketisheni watu. Palikuwako majani tele mahali pale. Bassi watu waume wakaketi, jumla yao wapata elfu tano.