John 6:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanafunzi walipokuwa wamekwenda umbali wa kilomita tano au sita, walimwona Yesu akitembea juu ya maji, anakaribia mashua; wakaogopa sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanafunzi walipokuwa wameenda mwendo wa maili tatu au nne, walimwona Isa akitembea juu ya maji akikaribia mashua, nao wakaogopa sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakavuta makasia kadiri ya maili tatu nne, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari na kukikaribia chombo; wakaogopa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakaiendesha mashua kiasi cha kilomita tano au sita. Kisha wakamwona Yesu. Yeye alikuwa anatembea juu ya maji, akiifuata mashua. Nao wakaogopa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wanafunzi walipokuwa wamekwenda umbali wa kilomita tano au sita, walimwona Yesu akitembea juu ya maji, anakaribia mashua; wakaogopa sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanafunzi walipokuwa wamekwenda umbali wa kilomita tano au sita, walimwona Yesu akitembea juu ya maji, anakaribia mashua; wakaogopa sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanafunzi walipokuwa wamekwenda mwendo wa karibu maili tatu au nne, walimwona Yesu akitembea juu ya maji akikaribia mashua, wakaogopa sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanafunzi walipokuwa wamekwenda mwendo wa karibu maili tatu au nne, walimwona Isa akitembea juu ya maji akikaribia mashua, nao wakaogopa sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakavuta makasia kadiri ya maili tatu nne, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari na kuikaribia mashua; wakaogopa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanafunzi walipokuwa wamekwenda umbali wa kilomita tano au sita, walimwona Yesu akitembea juu ya maji, anakaribia mashua; wakaogopa sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokwisha endelea mwendo wa nusu saa na kupita kidogo, wakamwona Yesu, anavyokwenda juu ya bahari na kukifikia chombo karibu, wakaogopa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakavuta makasia kadiri ya maili tatu nne, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari na kukikaribia chombo; wakaogopa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipofika umbali wa kadiri ya kilometre tano au sita, wakamwona Yesu anakaribia chombo, akitembea juu ya maji; kwa hiyo wakaogopa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wakavuta makasia kadiri ya stadio ishirini na tano au thelathini, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari, anakikaribia chombo: wakaogopa.