John 6:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi wakataka kumchukua Yesu katika mashua; na mara mashua ikawasili nchi kavu walikokuwa wanakwenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wakamkaribisha kwa furaha ndani ya mashua, na mara wakafika ufuoni walikokuwa wakienda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakataka kumpokea chomboni; na mara hiyo chombo kikaifikilia nchi waliyokuwa wakiiendea.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya kusema hivyo, wakamkaribisha kwenye mashua. Kisha mashua ikafika ufukweni katika sehemu waliyotaka kwenda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walifurahi kumchukua Yesu katika mashua; na mara mashua ikawasili nchi kavu walipokuwa wanakwenda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi wakataka kumchukua Yesu katika mashua; na mara mashua ikawasili nchi kavu walikokuwa wanakwenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo kwa furaha wakamkaribisha kwenye mashua, na mara wakafika walikokuwa wanakwenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo wakamkaribisha kwa furaha ndani ya mashua, na mara wakafika ufuoni walikokuwa wakienda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakataka kumpokea katika mashua; na mara hiyo mashua ikaifikia nchi waliyokuwa wakiiendea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi wakataka kumchukua Yesu katika mashua; na mara mashua ikawasili nchi kavu walikokuwa wanakwenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipotaka kumwingiza chomboni, mara chombo kikawa ufukoni kwenye nchi, walikokwenda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakataka kumpokea chomboni; na mara hiyo chombo kikaifikilia nchi waliyokuwa wakiiendea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wao walitaka kumupandisha ndani ya chombo lakini mara moja chombo kikafikia inchi kavu, pahali walipokuwa wakienda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wakataka kumpokea chomboni; na marra hiyo chombo kikaifikilia inchi waliyokuwa wakienda.