John 6:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake umati wa watu wale waliobaki upande wa pili wa ziwa walitambua kwamba kulikuwa na mashua moja tu pale, na Yesu hakuingia katika mashua pamoja na wanafunzi wake, ila wanafunzi hao walikuwa wamekwenda zao peke yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku iliyofuata, wale watu waliokuwa wamebaki ng’ambo waliona kwamba palikuwa na mashua moja tu, na kwamba Isa hakuwa ameondoka pamoja na wanafunzi wake, ila walikuwa wameondoka peke yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku ya pili yake mkutano waliosimama ng'ambo ya bahari waliona ya kuwa hakuna mashua nyingine huko ila moja, tena ya kuwa Yesu hakuingia katika mashua ile pamoja na wanafunzi wake, bali wanafunzi wake walikwenda peke yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku iliyofuata watu wengi walikuwa wamekaa upande mwingine wa ziwa. Nao walijua kuwa Yesu hakwenda pamoja na wafuasi wake kwenye mashua. Kwani walifahamu kuwa wafuasi wake waliondoka na mashua peke yao. Walijua pia kuwa ile ilikuwa ni mashua pekee iliyokuwepo pale.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kesho yake umati wa watu wale waliobaki upande wa pili wa ziwa walitambua kwamba kulikuwa na mashua moja tu pale, na Yesu hakuingia katika mashua pamoja na wanafunzi wake, ila wanafunzi hao walikuwa wamekwenda zao peke yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake umati wa watu wale waliobaki upande wa pili wa ziwa walitambua kwamba kulikuwa na mashua moja tu pale, na Yesu hakuingia katika mashua pamoja na wanafunzi wake, ila wanafunzi hao walikuwa wamekwenda zao peke yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku iliyofuata, wale watu waliokuwa wamebaki ng'ambo ya pili waliona kwamba palikuwepo na mashua moja tu na kwamba Yesu hakuwa ameondoka pamoja na wanafunzi wake, ila walikuwa wameondoka peke yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku iliyofuata, wale watu waliokuwa wamebaki ng’ambo waliona kwamba palikuwepo na mashua moja tu na kwamba Isa hakuwa ameondoka pamoja na wanafunzi wake, ila walikuwa wameondoka peke yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kesho yake mkutano waliosimama ng'ambo ya bahari waliona ya kuwa hakuna mashua nyingine huko ila moja, tena ya kuwa Yesu hakuingia katika mashua ile pamoja na wanafunzi wake, bali wanafunzi wake walikwenda peke yao,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake umati wa watu wale waliobaki upande wa pili wa ziwa walitambua kwamba kulikuwa na mashua moja tu pale, na Yesu hakuingia katika mashua pamoja na wanafunzi wake, ila wanafunzi hao walikuwa wamekwenda zao peke yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesho yake kundi la watu waliosimama ng'ambo ya bahari waliona, ya kuwa hakuwako chombo kingine huko, ni kile kimoja tu. Nao walikuwa wameona, ya kuwa Yesu hakuingia chomboni pamoja na wanafunzi wake; waliona, wanafunzi wake walivyoondoka peke yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku ya pili yake mkutano waliosimama ng’ambo ya bahari waliona ya kuwa hakuna mashua nyingine huko ila moja, tena ya kuwa Yesu hakuingia katika mashua ile pamoja na wanafunzi wake, bali wanafunzi wake walikwenda peke yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kesho yake watu waliobaki kule ngambo ya ziwa wakatambua kwamba kulikuwa tu chombo kimoja pale. Walijua vilevile kwamba Yesu hakuingia ndani ya chombo pamoja na wanafunzi wake, lakini wanafunzi wake walikwenda peke yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Siku ya pili yake makutano waliosimama ngʼambu ya bahari wakaona ya kuwa hakuna mashua nyingine huko illa ile moja waliyoingia wanafunzi wake; tena ya kuwa Yesu hakuingia katika mashua ile pamoja na wanafunzi wake, bali wanafunzi wake walikwenda peke yao,