John 6:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale watu walipomkuta Yesu ngambo ya pili wa ziwa walimwuliza, “Mwalimu, ulifika lini hapa?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipomkuta Isa ng’ambo ya bahari wakamuuliza, “Mwalimu, umefika lini huku?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata walipomwona ng'ambo ya bahari, walimwambia, Rabi, wewe umekuja lini hapa?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wakamwona Yesu akiwa upande mwingine wa ziwa. Wakamwuliza, “Mwalimu, ulifika huku lini?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wale watu walipomkuta Yesu ng'ambo ya pili wa ziwa walimwuliza, “Mwalimu, ulifika lini hapa?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale watu walipomkuta Yesu ng'ambo ya pili wa ziwa walimwuliza, “Mwalimu, ulifika lini hapa?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipomkuta Yesu ng'ambo ya bahari wakamwuliza, “Rabi, umefika lini huku?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipomkuta Isa ng’ambo ya bahari wakamuuliza, “Mwalimu, umefika lini huku?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata walipomwona ng'ambo ya bahari, walimwambia, Rabi, wewe umekuja lini hapa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale watu walipomkuta Yesu ngambo ya pili wa ziwa walimwuliza, “Mwalimu, ulifika lini hapa?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipomwona ng'ambo ya bahari wakamwuliza: Mfunzi mkuu, umefika lini hapa?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata walipomwona ng’ambo ya bahari, walimwambia, Rabi, wewe umekuja lini hapa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wale wakamukuta Yesu kule ngambo ya ziwa na kumwuliza: “Mwalimu, ulifika hapa wakati gani?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta walipomwona ngʼambu ya bahari, wakamwambia, Rabbi, umekuja lini hapa?