John 6:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msikishughulikie chakula kiharibikacho; kishughulikieni chakula kidumucho kwa ajili ya uhai wa milele. Mwana wa Mtu ambaye Baba amemthibitisha atawapeni chakula hicho.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba Mwenyezi amemtia muhuri.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini chakula cha kidunia kinaharibika na hakidumu. Ninyi msifanye kazi ili kupata chakula cha aina hiyo kinachoharibika. Isipokuwa fanyeni kazi ili mpate chakula kinachodumu na kinachowapa uzima wa milele. Mwana wa Adamu atawapa hicho chakula. Yeye ndiye pekee aliyethibitishwa na Mungu Baba kuwapa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Msikishughulikie chakula kiharibikacho; kishugulikieni chakula kidumucho kwa ajili ya uzima wa milele. Mwana wa Mtu ambaye Baba amemthibitisha atawapeni chakula hicho.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msikishughulikie chakula kiharibikacho; kishughulikieni chakula kidumucho kwa ajili ya uhai wa milele. Mwana wa Mtu ambaye Baba amemthibitisha atawapeni chakula hicho.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba amemtia muhuri.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba Mwenyezi amemtia muhuri.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msikishughulikie chakula kiharibikacho; kishughulikieni chakula kidumucho kwa ajili ya uhai wa milele. Mwana wa Mtu ambaye Baba amemthibitisha atawapeni chakula hicho.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sumbukieni vyakula! Lakini vile vinavyoangamia sivyo, ni vile vinavyokaa, viwafikishe penye uzima wa kale na kale, navyo ndivyo, Mwana wa mtu atakavyowapani ninyi. Kwani huyu ndiye, Baba Mungu aliyemwagiza hivyo na kumtia muhuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musitumikie chakula kinachoharibika, lakini mutumikie chakula kinachodumu na kuleta uzima wa milele. Mwana wa Mutu atawapa ninyi chakula hiki, kwa sababu Mungu Baba ametoa uhakikisho juu yake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hatta uzima wa milele, Mwana wa Adamu atakachowapeni: maana huyu ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.