John 6:34 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakamwambia, “Bwana, tupe daima mkate huo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamwambia, “Bwana, kuanzia sasa tupatie huo mkate siku zote.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wakasema, “Bwana, kuanzia sasa na kuendelea tupe mkate wa aina hiyo.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wakamwambia, “Mheshimiwa, tupe daima mkate huo.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakamwambia, “Bwana, tupe daima mkate huo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamwambia, “Bwana, kuanzia sasa tupatie huo mkate siku zote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamwambia, “Bwana Isa, kuanzia sasa tupatie huo mkate siku zote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakamwambia, Bwana, siku zote utupe chakula hiki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakamwambia, “Bwana, tupe daima mkate huo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipomwambia: Bwana, tupe siku zote mkate huo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wakamwambia: “Bwana, utupatie mukate ule siku zote.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, wakamwambia, Bwana, siku zote utupe mkate huo.