John 6:37 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wote anaonipa Baba watakuja kwangu; nami kamwe sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wote anipao Baba watakuja kwangu na yeyote ajaye kwangu, sitamfukuza nje kamwe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Vyote anavyonipa Baba vitakuja kwangu hata hivyo yeyote Yule atakayekuja kwangu sitamkataa kabisa. Nami kwa hakika daima nitawapokea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wote anaonipa Baba watakuja kwangu; nami sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wote anaonipa Baba watakuja kwangu; nami kamwe sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wote anipao Baba watakuja kwangu na ye yote ajaye kwangu, sitamfukuzia nje kamwe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale wote anipao Baba watakuja kwangu na yeyote ajaye kwangu, sitamfukuzia nje kamwe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wote anaonipa Baba watakuja kwangu; nami kamwe sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wote, Baba anipao, ndio watakaokuja kwangu; naye ajaye kwangu sitamfukuza, ajiendee.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wote Baba anaonipa wanakuja kwangu; nami sitamukataa hata kidogo yule anayekuja kwangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe.