John 6:42 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakasema, “Je, huyu si mwana wa Yosefu? Tunamjua baba yake na mama yake! Basi, anawezaje kusema kwamba ameshuka kutoka mbinguni?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakasema, “Huyu si Isa, mwana wa Yusufu, ambaye baba yake na mama yake tunawajua? Anawezaje basi sasa kusema, ‘Nimeshuka kutoka mbinguni’?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakasema, Je! Huyu siye Yesu, mwana wa Yusufu, ambaye twamjua babaye na mamaye? Sasa asemaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakasema, “Huyu ni Yesu. Tunawajua baba na mama yake. Yeye ni mtoto wa Yusufu. Anawezaje kusema, ‘Nilishuka kutoka mbinguni’?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakasema, “Je, huyu si mwana wa Yosefu? Tunawajua baba yake na mama yake! Basi, anawezaje kusema kwamba ameshuka kutoka mbinguni?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakasema, “Je, huyu si mwana wa Yosefu? Tunamjua baba yake na mama yake! Basi, anawezaje kusema kwamba ameshuka kutoka mbinguni?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakasema, “Huyu si Yesu, mwana wa Yosefu, ambaye baba yake na mama yake tunawajua? Anawezaje basi sasa kusema, ‘Nimeshuka kutoka mbinguni’?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakasema, “Huyu si Isa, mwana wa Yusufu, ambaye baba yake na mama yake tunawajua? Anawezaje basi sasa kusema, ‘Nimeshuka kutoka mbinguni’?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakasema, Je! Huyu siye Yesu, mwana wa Yusufu, ambaye twamjua babaye na mamaye? Sasa asemaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakasema, “Je, huyu si mwana wa Yosefu? Tunamjua baba yake na mama yake! Basi, anawezaje kusema kwamba ameshuka kutoka mbinguni?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakasema: Huyu siye Yesu, mwana wa Yosefu? Hatumjui baba yake na mama yake? Asemaje sasa: Nimeshuka toka mbinguni?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakasema, Je! Huyu siye Yesu, mwana wa Yusufu, ambaye twamjua babaye na mamaye? Sasa asemaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakasema: “Huyu si Yesu mwana wa Yosefu? Si tunawajua baba yake na mama yake? Namna gani anaweza kusema sasa kwamba alishuka toka mbinguni?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakanena, Huyu siye Yesu, mwana wa Yusuf, ambae twamjua baba yake na mama yake? Bassi, anenaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?