John 6:58 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, huu ndio mkate ulioshuka kutoka mbinguni; si kama mana waliyokula babu zenu, wakafa. Aulaye mkate huu atakuwa hai milele.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mimi siyo kama ule mkate walioula baba zenu. Wao waliula mkate huo, lakini bado walikufa baadaye. Mimi ni mkate uliotoka mbinguni. Yeyote atakayeula mkate huu ataishi milele.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, huu ndio mkate ulioshuka kutoka mbinguni; si kama mana waliyokula babu zetu, wakafa. Aulaye mkate huu ataishi milele.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, huu ndio mkate ulioshuka kutoka mbinguni; si kama mana waliyokula babu zenu, wakafa. Aulaye mkate huu atakuwa hai milele.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, huu ndio mkate ulioshuka kutoka mbinguni; si kama mana waliyokula babu zenu, wakafa. Aulaye mkate huu atakuwa hai milele.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huo ndio mkate ulioshuka toka mbinguni, si kama ile, baba zenu waliyoila, wakafa. Mwenye kuula mkate huu atakuwa mzima pasipo mwisho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huu ndio mukate ulioshuka toka mbinguni, nao si kama mukate ule babu zenu waliokula katika jangwa na kufa. Anayekula mukate huu ataishi milele.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Huu ni mkale ulioshuka kutoka mbinguni; si kama baba zenu walivyoila manna wakafa; aulae mkate huu ataishi milele.