John 6:63 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Roho ndiyo iletayo uhai; mwili hauwezi kitu. Maneno niliyowaambia ni roho na uhai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Roho ndiye atiaye uzima, mwili haufai kitu. Maneno haya niliyowaambia ni Roho tena ni uzima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Roho ndiye anayeleta uzima. Sio mwili. Lakini maneno niliyowaambia yanatoka kwa Roho, hivyo yanaleta uzima.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Roho ndiye atiaye uzima; binadamu peke yake hawezi. Maneno niliyowaambieni ni Roho, ni uzima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Roho ndiyo iletayo uhai; mwili hauwezi kitu. Maneno niliyowaambia ni roho na uhai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Roho ndiye atiaye uzima, mwili haufai kitu. Maneno haya niliyowaambia ni Roho tena ni uzima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Roho ndiye atiaye uzima, mwili haufai kitu. Maneno haya niliyowaambia ni Roho tena ni uzima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Roho ndiyo iletayo uhai; mwili hauwezi kitu. Maneno niliyowaambia ni roho na uhai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Roho ndiyo inayotupatia uzima, mwili haufai kitu. Maneno, niliyowaambia, ndiyo ya Kiroho yenye uzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Roho ndiye anayeleta uzima; mwili hauwezi kufaa kitu. Maneno haya niliyosema nanyi, ndiyo Roho na uzima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Roho ndiyo itiayo uzima; mwili haufai kitu; maneno ninayowaambieni ni roho, tena ni uzima.