John 6:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Yupo hapa mtoto mmoja aliye na mikate mitano ya shayiri na samaki wawili; lakini hivi vyatosha nini kwa watu wengi kama hawa?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa watu hawa wote?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Yupo hapa kijana mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wadogo wawili. Lakini hiyo haitoshi kwa umati huu wa watu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Yupo hapa mtoto mmoja aliye na mikate mitano ya shayiri na samaki wawili; lakini hivi vyatosha nini kwa watu wengi kama hawa?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Yupo hapa mtoto mmoja aliye na mikate mitano ya shayiri na samaki wawili; lakini hivi vyatosha nini kwa watu wengi kama hawa?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa umati wote huu?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa umati huu wote?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yupo hapa mtoto, ana mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Yupo hapa mtoto mmoja aliye na mikate mitano ya shayiri na samaki wawili; lakini hivi vyatosha nini kwa watu wengi kama hawa?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapa yupo mtoto mdogo, anayo mikate mitano ya mofa na visamaki viwili. Lakini hivyo vitawafaa nini watu walio wengi kama hawa?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Hapa kuna mutoto mumoja anayekuwa na mikate mitano ya shayiri pamoja na samaki mbili. Lakini chakula hiki hakitawafalia kitu watu wengi kama hawa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yupo mtoto hapa, ana mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini haya nini kwa watu wengi kama hivi?