John 7:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulikuwa na minongono mingi katika umati wa watu. Baadhi yao walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “La! Anawapotosha watu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kulikuwa na minong’ono iliyoenea kumhusu Isa katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kukawa na manung'uniko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lilikuwepo kundi la watu wengi mahali pale. Wengi kati yao walikuwa wakizungumza kwa siri kuhusu Yesu. Wengine wakasema, “Huyu ni mtu mzuri.” Lakini wengine wakakataa na kusema, “Hapana, mtu huyo huwadanganya watu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulikuwa na minong'ono mingi katika umati wa watu. Baadhi yao walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “La! Anawapotosha watu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulikuwa na minong'ono mingi katika umati wa watu. Baadhi yao walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “La! Anawapotosha watu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kulikuwa na minong'ono iliyoenea kumhusu Yesu katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kulikuwa na minong’ono iliyoenea kumhusu Isa katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kukawa na manung'uniko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulikuwa na minongono mingi katika umati wa watu. Baadhi yao walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “La! Anawapotosha watu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kukawa na manung'uniko mengi katika makundi ya watu kwa sababu yake. Wengine walisema: Ni mtu mwema; wengine walisema: Sio, ila hupoteza watu tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kukawa na manung’uniko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika kundi lile kulikuwa manunguniko mengi juu yake. Wamoja walisema: “Yeye ni mutu muzuri.” Wengine walisema: “Hapana, si vile, yeye anawadanganya watu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kukawa manungʼuniko mengi katika makutano kwa khabari zake; wengine wakisema, Yu mtu mwema; na wengine wakisema, Sivyo, bali anawadanganya makutano.