John 7:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose aliwapeni ile desturi ya kutahiri. (Si kwamba desturi hiyo ilitoka kwa Mose, bali ilitoka kwa mababu). Sasa nyinyi humtahiri mtu hata siku ya Sabato.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kwa kuwa Musa aliwaamuru tohara (ingawa kwa kweli haikutoka kwa Musa bali kwa baba zetu wa zamani), mnamtahiri mtoto hata siku ya Sabato.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi siku ya sabato humtahiri mtu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mnatii sheria aliyowapa Musa kuhusu kutahiriwa; nanyi mnatahiri hata siku ya Sabato! (Lakini hakika, Musa siye aliyewatahiri. Tohara Ilitoka kwa baba zenu walioishi kabla ya Musa.) Ndiyo, siku zote mnatahiri wana wenu hata siku ya Sabato.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mose aliwapeni ile desturi ya kutahiri. (Si kwamba desturi hiyo ilitoka kwa Mose, bali ilitoka kwa mababu). Sasa ninyi humtahiri mtu hata siku ya Sabato.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose aliwapeni ile desturi ya kutahiri. (Si kwamba desturi hiyo ilitoka kwa Mose, bali ilitoka kwa mababu). Sasa nyinyi humtahiri mtu hata siku ya Sabato.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kwa kuwa Mose aliwaamuru tohara (ingawa kwa kweli haikutoka kwa Mose bali kwa baba zenu wakuu), mnamtahiri mtoto hata siku ya Sabato.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kwa kuwa Musa aliwaamuru tohara (ingawa kwa kweli haikutoka kwa Musa bali kwa baba zenu wakuu), mnamtahiri mtoto hata siku ya Sabato.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi mwatahiri mtu siku ya sabato.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose aliwapeni ile desturi ya kutahiri. (Si kwamba desturi hiyo ilitoka kwa Mose, bali ilitoka kwa mababu). Sasa nyinyi humtahiri mtu hata siku ya Sabato.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hiyo Mose aliwaagiza kutahiri watu; tena siye Mose aliyeviagiza, ila baba zenu. Nanyi humtahiri mtu hata siku ya mapumziko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi siku ya sabato humtahiri mtu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi munatahiri watu hata kwa siku ya Sabato kwa sababu Musa aliwatolea ninyi amri ya kutahiri, (kwa hakika haikutoka kwa Musa, lakini kwa babu zenu).
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu hii Musa aliwapa tohara, si kwamba yatoka kwa Musa bali kwa babu zenu: nanyi siku ya sabato humtahiri mtu.