John 7:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikiwa basi, mtu hutahiriwa hata siku ya Sabato kusudi sheria isivunjwe, mbona mnanikasirikia kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya Sabato?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa mtoto aweza kutahiriwa siku ya Sabato kusudi Torati ya Musa isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia kwa kumponya mtu mwili wake wote siku ya Sabato?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii inaonesha kuwa mtu anaweza kutahiriwa siku ya Sabato ili kuitimiza sheria ya Musa. Sasa kwa nini mnanikasirikia mimi kwa kuuponya mwili wote wa mtu siku ya Sabato?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ikiwa basi, mtu hutahiriwa hata siku ya Sabato kusudi Sheria ya Mose isivunjwe, mbona mnanikasirikia kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya Sabato?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikiwa basi, mtu hutahiriwa hata siku ya Sabato kusudi sheria isivunjwe, mbona mnanikasirikia kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya Sabato?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa mtoto aweza kutahiriwa siku ya Sabato kusudi sheria ya Mose isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia kwa kumponya mtu mwili wake wote siku ya Sabato?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa mtoto aweza kutahiriwa siku ya Sabato kusudi Torati ya Musa isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia kwa kumponya mtu mwili wake wote siku ya Sabato?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ikiwa mtu hupaswa tohara siku ya sabato, ili Torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nilimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikiwa basi, mtu hutahiriwa hata siku ya Sabato kusudi sheria isivunjwe, mbona mnanikasirikia kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya Sabato?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akitahiriwa siku ya mapumziko, kwamba Maonyo ya Mose yasivunjwe, mbona mnanikasirikia mimi, kwa sababu nimeponya mwili wote wa mtu siku ya mapumziko?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, kama munaweza kutahiri mutu kwa siku ya Sabato, kusudi musivunje Sheria ya Musa, kwa nini munanikasirikia kwa sababu nimemuponyesha mutu kabisa kwa siku ya Sabato?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi ikiwa mtu apashwa tohara siku ya sabato, torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato?